Matukio-picha

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA KITAIFA WA BARAZA LA AFRICA KUHUSU UFUMBUZI WA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI KATIKA NGAZI ZA SERIKALI ZA MITAA

JINA LA MKUTANO: PAN AFRICAN CONGRES
MGENI RASMI: MH: RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KAULI MBIU "KUWA SEHEMU YA UFUMBUZI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UKUAJI WA MIJI, MIUNDOMBINU NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI BARANI AFRICA"
WENYEJI WA MKUTANO: JIJI LA DAR ES SALAAM, BARAZA LA KIMATAIFA LA SERIKALI ZA MITAA LA KUSIMAMIA MAZINGIRA (ICLEI) NA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA (ALAT)
WASHIRIKI WA MKUTANO: MASHIRIKA YA KIMATAIFA, MAKAMPUNI, TASISI, VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA
DHUMUNI LA MKUTANO: KUJENGA MTANDAO WA PAMOJA WA UJENZI WA MIJI SALAMA, YENYE MIUNDOMBINU YA KUAMINIKA NA MIFUMO YA KIJAMII YA KULETA MAENDELEO NA USATAWI ENDELEVU.
MASHIRIKA NA TASISI ZITAKAZOHUDHURIA: ALAT, NEPAD, AMCOW, UCLGA, UNDP, UNISDR, UN-HABITAT, UNEP, FAO, OXFAM, IDRC, CDKN, GIZ, UNIVERSITIES NA NGOS
TAREHE YA MKUTANO: 30-10-2013 HADI 01-11-2013
WANAOHITAJI KUDHAMINI MKUTANO: WASILIANA NASI KUPITIA www.locs4africa.org au tuma email : locs4africa@iclei.org au alat_tz@yahoo.com

Mhe.Dkt. Didas J. Massaburi Meya wa jiji la Dar es salaam akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng. Mussa Natty wakati wakiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano mkubwa wa mazingira utakaofanyika jijini Dar es salaam , Mkutano huo utahusu Ufumbuzi wa mabadiliko ya tabia ya nchi katika ngazi za serikali za mitaa. 


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng. Mussa Natty akiteta jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari hivi leo kuhusiana na mkutano mkubwa utakaofanyika hapa jijini.






MALIPO KWA NJIA YA MTANDAO MBIONI KUANZA KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

katika kutimiza azima ya  kuongeza mapato na kuimarisha ukusanyaji mapato kwa kutumia  serikali Mtandao (e-governce) Manispaa ya Kinondoni chini ya Mkurugenzi wake  Eng. Musa Natty akisaidiana na Timu ya Watendaji  wote wa Halmashauri ya Manispaa  na Wafanya maamuzi  katika Manispaa chini ya uongozi wa Mstahiki meya Yusuph Mwenda, Halmashauri ipo  katika hatua za mwisho kabisa za kuanza kufanya malipo ya Kodi zote za Halmashauri  kwa njia ya Mtandao. Kampuni ambayo imeshinda zabuni ya kufanya shughuli hii  imeshapatikana  kwa jina inajulikana kuwa ni  MAXMALIPO .
Baada ya zoezi la kuhuisha mifumo kukamilika Mwananchi ataweza kulipia kodi zote kupitia simu za Kiganjani (Mobile phone) katika mitandao ifuatayo - Vodacom-M-pesa, Airtel -Airtel - Air tel money na Tigo-Tigo pesa 
Njia hii rahisi  itasaida  mlipaji wa kodi kutumia muda mfupi kufanya malipo ya kodi yake  ndani ya Manispaa ya  Kinondoni  na vilevile itapunguza kero na upotevu wa kodi ambao ulikuwa hauwezi kuzuilika.  Lengo  la Halmashauri ni kuongeza mapato kwa kiwango cha juu  katika ukusanyaji na baadaye kuweza kufikia lengo kuu la huduma bora kwa wananchi.

 Leo tarehe 13/09/2013 Halmshauri imekutana na  viongozi wa ngazi za mitaa ambao ni  wenyekiti wa serikali za mitaa  wakiambatana na Watendaji wa kata na mitaa pamoja na  wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri ili waweze kutoa maoni yao kuhusu teknolojia hii mpya ya ulipaji wa kodi kwa njia mitandao kwa kodi zote za Halmashauri.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng. Musa Natty akiwakaribisha washiriki wa mkutano wa kujadili njia mbadala yaulipaji kodi katika manispaa ya kinondoni, ambapo muda si mrefu Kodi zote za Halmashauri zitaanza kulipwa kwa njia ya Mitandao ya simu na vituo vya malipo maxmalipo. kushoto kwake ni DAS wa wilaya ya kinondoni




Mhasibu wa mapato wa manispaa ya kinondoni Ndugu Mwaikatare akisikiliza kwa makini maelezo ya jinsi gani kampuni ya maxmalipo itaiwezesha manispaa kukusanya zaidi kwa kutumia mifumo ya kompyuta

Wenyekiti wa Serikali za mitaa katika wilaya ya kinondoni wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa pili toka kulia aliyevaa miwani wakiwa tayari kusikiliza maelezo toka maxmalipo jinsi manispaa itakavyokusanya kodi zake kwa njia ya mtandao

Wenyekiti wa Mitaa pamoja na watendaji wa mitaa wakisikiliza kwa makini sana kutoka kwa mkurugenzi wa maxmalipo jinsi makusanyo ya kodi yatakavyofanywa kwa njia ya mtandao. 

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama katika manispaa ya kinondoni wakiwa makini  kusikiliza maelezo toka mkurugenzi wa maxmalipo jinsi manispaa itakavyokusanya kodi zake kwa njia ya mtandao
Mwisho kushoto ni Ndugu Godfrey H. Mgomi Afisa utumishi mkuu wa Manispaa ya kinondoni akiwa na meneja wa ICT katika manispaa mama k Veronica Igoko kushoto kwake aliyeinamisha kichwa wakisikiliza kwa makini jinsi manispaa itakavyokuza kipato cha kodi kwa njia hii mpya ya ukusanyaji kodi kwa Mtandao.

Mkurugenzi wa Maxmalipo akiwa anatoa maelezo ya jinsi maxmalipo watakavyoiwezesha manispaa kukeusanya kodi zote kwa njia ya mtandao.
Naibu meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Songoro Mnyonge, Mkurugenzi wa manispaa na Mwenyekiti wa Wenyekiti wa mitaa wakifuatilia kwa makini maelezo toka maxmalipo jinsi manispaa itakavyokusanya kodi zake kwa njia ya mtandao






















MAKABIDHIANO YA MIUNDO MBINU YA USALAMA BARABARANI KATIKA SHULE YA MSINGI MIANZINI


























ZIARA YA VIONGOZI  MANISPAA YA KINONDONI NCHINI BRAZILI  WIKI ILIYOPITA


Hii ni siku ya ufunguzi ambapo ujumbe kutoka Manispaa ya kinondoni ukiongozwa na Naibu meya Mh Songoro Mnyonge  pamoja na Afisa utumishi mkuu ndugu Godfrey Mgomi pamoja na wageni wengine kutoka Nchi za marekani, Ghana na Togo walikuwa wakikaribishwa na mwenyeji wao ambaye ni meya wa jiji la  Belo Horizonte huko Nchini brazil barani America kwa ajili ya ziara ya uhifadhi wa chakula (food security study tour)

Hawa nidio waliokuwa wenyeji wetu huko  Belo Horizonte Nchini Brazil bara la America  

ujumbe ulioitembelea brazil kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania tuliwakilishwa na Afisa utumishi mkuu wa manispaa ya Kinondoni  ndugu Godfrey Mgomi na Naibu Meya wa kinondoni Mh Songoro Mnyonge, wakiwa katika picha ya pamoja tunashukuru kwa uwakilishwaji wa manispaa yetu ya kinondoni huko barani America

 
Wahandisi wa  Belo Horizonte wakitoa maelezo ya jinsi wanavyofanya shughuli zao za mipango miji kwa wajumbe kutoka Nchi mbalimbali waliotembelea Brasil kwa ajili ya kujionea na kujifunza mambo mbalimbali likiwemo swala la uhifadhi wa chakula na uongozi Kulia nyuma ni Afisa utumishi mkuu ndugu Godfrey Mgomi na aliyevaa koti ya rangi ya maziwa na Naibu meya wa manispaa ya kinondoni Mh. songoro Mnyonge pamoja na wajumbe wengine kutoka Marekani, Togo, ghana n,k


Hapa Wahandisi wa jiji la  Belo Horizonte wakiwaonyesha wajumbe jinsi walivyoupangilia mji wao baada ya kupewa idhini na serikali.

ZIARA YA KAMATI NDOGO YA BUNGE KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

Kamati ndogo ya bunge kuhusu mambo ya TAMISEMI ikipokelewa jana katika viwanja vya Manispaa ya Kinondoni tayari kwa kuanza kazi ya kukagua miradi ya Maendeleo katika  Manispaa ya Kinondoni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng Mussa Natty akiwaongoza Wajumbe wa kamati kuelekea katika ukumbi wa mikutano- manispaa

Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni MhYusuph Mwenda akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya ukaguzi TAMISEMI Mh. Machali

Wajumbe wa Kamati wakifuatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya kinondoni

Eng. Mussa Natty akiwa anatoa taarifa ya utekelezaji katika Manispaa ya kinondoni

Wajumbe wa kamati ya TAMISEMI wakiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika hospitali ya Mwananyamala






Picha mbalimbali zikionyesha tukio futari liliofanyika katika viwanja vya manispaa ya kinondoni
ambapo Mstahiki Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda aliwaalika watu mbalimbali katika futari hiyo kama inavyoonekana katika picha. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Slaa, Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Ndugu Reginald Mengi na watu wengine mashuhuri waliudhuria
Mstahiki meya Akiwa anaongea jambo katika Futari hiyo, kushoto ni Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Mh Jery Slaa na Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP ndugu  Reginald Mengi.
 


























0 comments:

Post a Comment